Lengo la Hizb ut Tahrir
Lengo lake ni kurejesha mfumo wa maisha wa Kiislamu na kuufikisha ulinganizi wa Kiislamu (da’wah) ulimwenguni. Lengo hili linamaanisha kuwarudisha Waislamu kuishi maisha ya Kiislamu katika Dar al-Islam na katika jamii ya Kiislamu ili mambo yote ya maisha katika jamii yaendeshwe kulingana na sheria za Shari’ah, na mtazamo ndani yake uwe ni halali na haramu chini ya kivuli cha Dola ya Kiislamu, ambayo ni Dola ya Khilafah. Dola hiyo ni ile ambayo Waislamu wanamteua Khalifa na kumpa bay’ah ya kusikiliza na kutii kwa sharti kwamba atawale kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kwa sharti kwamba aufikishe Uislamu kama ujumbe kwa ulimwengu kupitia da’wah na jihad.
Chama, pia, kinalenga ufufuo sahihi wa Ummah kupitia fikra iliyoelimika. Pia kinajitahidi kuurudisha kwenye nguvu na utukufu wake wa zamani ili unyakue hatamu za uanzilishi kutoka kwa mataifa na dola nyingine, na kurejea kwenye nafasi yake ya haki kama dola ya kwanza ulimwenguni, kama ilivyokuwa huko nyuma, inapoitawala dunia kulingana na sheria za Uislamu.
Pia inalenga kurejesha mwongozo wa Kiislamu kwa wanadamu na kuuongoza Ummah katika mapambano na Kufru, mifumo yake na fikra zake ili Uislamu ufunike ulimwengu.