Hizb ut Tahrir

Hizb ut-Tahrir ni chama cha kisiasa ambacho itikadi yake ni Uislamu, hivyo siasa ni kazi yake na Uislamu ni itikadi yake. Kinafanya kazi ndani ya Ummah na pamoja nao, ili kwamba uuchukue Uislamu kama suala lake kuu na uongozwe kurejesha Khilafah na kuhukumu kwa kile alichokiteremsha Mwenyezi Mungu (swt).

Asili ya Chama

Hizb ut-Tahrir ni kundi la kisiasa na wala si kundi la kikuhani. Wala si kundi la kitaaluma, kielimu au la hisani. Fikra ya Kiislamu ndiyo roho ya mwili wake, kiini chake na siri ya uhai wake.