Njia ya Hizb ut-Tahrir

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Njia iliyochukuliwa na Hizb ut-Tahrir kufikisha da’wah ni Sheria ya Shari’ah iliyotokana na seerah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika utendaji wake wakati wa ufikishaji wa da’wah. Hii ni kwa sababu ni wajibu kumfuata yeye, kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyosema:

“Hakika nyinyi mnacho kiigizo chema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana.” [TMQ 33:21]

“Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu.” [TMQ 3:31]

“Na anachokupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho.” [TMQ 59:7]

Kuna aya nyingine nyingi kama hizi zinazoashiria kwamba kumfuata Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kumchukua kama mfano na kuchukua vipengele vyote vya dini kutoka kwake ni wajibu.

Kwa kuwa Waislamu siku hizi wanaishi katika Dar al-Kufr, kwa sababu wanatawaliwa na sheria nyingine isipokuwa ufunuo wa Mwenyezi Mungu (swt), hivyo ardhi yao inafanana na Makkah ambapo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitumwa kwa mara ya kwanza kama Mtume. Kwa hivyo, ni muhimu kuchukua sehemu ya Makkah ya seerah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kama mfano katika kufikisha da’wah.

Kwa kusoma maisha ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akiwa Makkah mpaka alipo (saw) alipofanikiwa kusimamisha Dola ya Kiislamu Madinah, ni dhahiri kwamba yeye (saw) alipitia hatua zilizofafanuliwa wazi, ambapo katika kila moja yeye (saw) alikuwa akifanya vitendo maalum vilivyowazi. Kwa hivyo Chama kilichukua kutoka hapo njia ya utendaji, hatua za utendaji wake na vitendo ambavyo inapaswa kuvifanya katika hatua hizi kulingana na vitendo ambavyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivifanya wakati wa hatua za kazi yake.

Hatua Tatu

Kulingana na hili, Chama kilifafanua njia yake ya kazi katika hatua tatu:

  1. Hatua ya Kwanza: Hatua ya kuelimisha (culturing) ili kuzalisha watu wanaoamini katika wazo na njia ya Chama, ili waunde kundi la Chama.
  2. Hatua ya Pili: Hatua ya kuingiliana na Ummah, ili kuuacha Ummah ukumbatie na kubeba Uislamu, ili Ummah uuchukue kama suala lake, na hivyo kufanya kazi kuusimamisha katika mambo ya maisha.
  3. Hatua ya Tatu: Hatua ya kusimamisha serikali, kutekeleza Uislamu kwa ujumla na kikamilifu, na kuubeba kama ujumbe kwa ulimwengu.

Hatua ya Kwanza

Chama kilianza hatua ya kwanza huko Al-Quds mwaka 1372 AH (1953 CE) chini ya uongozi wa mwanzilishi wake, mwanachuoni mtukufu, mfikiriaji, mwanasiasa hodari, kadhi katika Mahakama ya Rufaa huko Al-Quds, Taqiuddin an-Nabahani (rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake). Katika hatua hii, Chama kilikuwa kikiwasiliana na wanachama wa Ummah, kikiwasilisha kwao, kwa msingi wa mtu mmoja mmoja, wazo na njia yake. Yeyote aliyekubali wazo la msingi, Chama kilimuandalia masomo ya kina katika halqa (duara) za Chama, ili atakasike kwa mawazo na sheria za Uislamu zilizochukuliwa na Chama na hivyo katika mchakato huo kuwa haiba ya Kiislamu. Hivyo anaingiliana na Uislamu na kufurahia fikra za Kiislamu na hisia za Kiislamu zinazompelekea kuanza kubeba da’wah kwa watu. Mtu anapofikia hatua hii anajilazimisha kwa Chama na hivyo kuwa mwanachama wake.

Hii ndiyo njia ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitenda katika hatua yake ya kwanza ya da’wah, ambayo iliendelea kwa miaka mitatu, kwa kuwalingania watu mmoja mmoja na kuwasilisha kwao yale ambayo Mwenyezi Mungu (swt) alimteremshia yeye (saw). Aliwakusanya pamoja kwa siri wale waliomwamini kwa msingi wa itikadi hii. Alikuwa na shauku ya kuwafundisha Uislamu na kuwasomea yale yaliyoteremshwa na yaliyokuwa yakiteremshwa kwake mpaka alipowayeyusha na Uislamu. Alikuwa akikutana nao kwa siri na kuwafundisha katika sehemu zilizofichika kutoka kwa macho ya watu. Pia walikuwa wakifanya ibada zao kwa kujificha. Hatimaye, da’wah ya Uislamu ilienea Makkah, na watu walianza kuizungumzia na kuanza kuingia katika Uislamu kwa makundi.

Katika hatua hii ya da’wah, Chama kilielekeza umakini wake katika kujenga mwili wake, kuongeza wanachama wake na kuelimisha watu binafsi katika halqa zake kwa utamaduni wa Chama uliokolea mpaka kilipofanikiwa kuunda muundo wa chama kutoka kwa watu waliyeyushwa na Uislamu, na ambao walikuwa wamechukua mawazo ya Chama na walikuwa wameingiliana na mawazo haya na kuyafikisha kwa watu. Baada ya Chama kufanikiwa kuunda muundo wake na jamii ikawa inakifahamu, ikakitaambua na mawazo yake na kile kinacholingania, Chama kilihamia hatua ya pili.

Hatua ya Pili

Hatua hii ni mwingiliano na Ummah ili kuufanya ubebe Uislamu na kusimamisha katika Ummah ufahamu wa pamoja na maoni ya umma juu ya mawazo na sheria za Uislamu zilizochukuliwa na Chama, ili uyachukue kama mawazo yake wenyewe na kujitahidi kuyasimamisha katika maisha, na kuendelea na Chama katika kazi ya kusimamisha Dola ya Khilafah na kumteua Khaleefah ili kurejesha njia ya maisha ya Kiislamu na kubeba da’wah ya Kiislamu kwa ulimwengu.

Katika hatua hii Chama kiliendeleza shughuli zake kutoka kuwafikia watu binafsi tu hadi kuzungumza na umma kwa pamoja. Katika hatua hii kilikuwa kikitekeleza kazi zifuatazo:

  1. Uelimishaji uliokolea wa watu binafsi katika halqa ili kujenga mwili wa Chama na kuongeza wanachama wake, na kuzalisha haiba za Kiislamu ambazo zina uwezo wa kufikisha da’wah na kukimbilia mbele katika mapambano ya kifikra na kisiasa.

  2. Uelimishaji wa pamoja wa umma wa Ummah kwa mawazo na sheria za Uislamu ambazo Hizb imezichukua, kupitia masomo, mihadhara, na mazungumzo misikitini, vituoni na sehemu za mikutano ya kawaida, na kupitia vyombo vya habari, vitabu na vipeperushi. Hii ilifanywa ili kuunda ufahamu wa pamoja ndani ya Ummah na kuingiliana nao.

  3. Mapambano ya kifikra dhidi ya itikadi, mifumo na mawazo ya Kikafiri, mawazo potofu na dhana za ulaghai kwa kufichua ubatili wao, kasoro na mgongano wao na Uislamu, ili kuukomboa Ummah kutoka kwao na kutoka kwa athari zao.

  4. Mapambano ya kisiasa, ambayo yanawakilishwa na yafuatayo:

    • Mapambano dhidi ya mataifa ya kikoloni ya Kikafiri ambayo yana utawala na ushawishi katika nchi za Kiislamu. Changamoto dhidi ya ukoloni katika aina zake zote za kifikra, kisiasa, kiuchumi na kijeshi, inahusisha kufichua mipango yake, na kufichua njama zake ili kuukomboa Ummah kutoka kwa udhibiti wake na kuuweka huru kutoka kwa athari yoyote ya ushawishi wake.

    • Mapambano dhidi ya watawala katika nchi za Kiarabu na Kiislamu, kwa kuwafichua, kuwawajibisha, kuchukua hatua kuwabadilisha wakati wowote walipokataa haki za Ummah au walipopuuza kutekeleza wajibu wao kwake, au walipopuuza jambo lolote la mambo yake, na wakati wowote walipotofautiana na sheria za Uislamu, na kuchukua hatua pia kuondoa tawala zao ili kusimamisha utawala wa Kiislamu mahali pake.

  5. Kuchukua maslahi ya Ummah na kuchukua mambo yake kwa mujibu wa sheria za Shari’ah.

Chama kimetekeleza kazi hii yote kikifuata yale ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alifanya baada ya Mwenyezi Mungu (swt) kumteremshia:

“Basi tangaza uliyo amrishwa, na jitenge na washirikina.” [TMQ 15:94]

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitangaza ujumbe wake na akaalika Maquraishi kwenye Mlima Safa na kuwaambia kwamba yeye ni Mtume aliyetumwa kwao. Aliwataka wamuamini. Alianza kufanya wito wake kwa umma na pia kwa watu binafsi. Maquraishi walipompinga, aliwakabili Maquraishi, miungu yao ya uongo, itikadi na mawazo, akielezea ubatili wao, ufisadi na kasoro. Aliwakashifu na kuwashambulia kama alivyoshambulia itikadi na mawazo yote ya uongo yaliyokuwepo. Aya za Qur’an ziliteremshwa kwake mfululizo juu ya masuala haya na zilikemea vitendo vya Maquraishi vya kula riba, kuzika binti zao wakiwa hai, upimaji wa ulaghai na zinaa. Aya pia ziliteremshwa zikiwashambulia viongozi na wakuu wa Maquraishi, zikiwatukana wao, mawazo yao na baba zao, na kufichua njama zao dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na dhidi ya da’wah yake na Maswahaba zake.

Chama kilikuwa wazi, wazi na chenye changamoto katika kubeba mawazo yake na katika kukabiliana na mawazo ya uongo na vyama vya kisiasa, katika mapambano yake dhidi ya wakoloni makafiri na katika mapambano yake dhidi ya watawala. Hakipendekezi, hakibembelezi, hakitendi kwa adabu au kupendelea usalama, bila kujali matokeo au mazingira ya da’wah yake. Kinatoa changamoto kwa kila mtu anayetofautiana na Uislamu na sheria zake, jambo ambalo limekiweka wazi kwa madhara makubwa yaliyofanywa na watawala dhidi yake; kama vile kifungo, mateso, kufukuzwa, kufuatiliwa, kushambuliwa kwa riziki za wanachama, kuharibiwa kwa maslahi, kupigwa marufuku kusafiri na mauaji. Watawala dhalimu nchini Iraq, Syria, Libya na wengine wameua makumi ya wanachama wake. Magereza ya Jordan, Syria, Iraq, Misri, Libya na Tunisia yamejaa wanachama wake.

Chama kilihimili yote haya kwa kufuata mfano wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Alikuwa yeye (saw) aliyekuja na Ujumbe wa Uislamu kwa ulimwengu wote. Aliupa changamoto kwa njia ya wazi, akiamini katika ukweli ambao yeye (saw) aliulingania. Yeye (saw) aliupa changamoto ulimwengu wote, akipambana na wote na kila mtu, bila kujali tabia zao, mila, dini, itikadi, watawala au watu wa kawaida. Hakutilia maanani kidogo chochote isipokuwa Ujumbe wa Uislamu. Alichukua hatua dhidi ya Maquraishi kwa kukashifu miungu yao. Aliwapa changamoto kuhusu imani zao na aliwatukana wakati alikuwa mtu mmoja tu, bila njia za kutosha au wasaidizi, na hakuwa na silaha isipokuwa Iman yake ya kina katika Ujumbe wa Uislamu ambao yeye (saw) alitumwa nao.

Ingawa Chama kilijitolea kuwa wazi, wazi na chenye changamoto katika da’wah yake, kilijizuia kwa vitendo vya kisiasa pekee na hakikuvuka mipaka kwa kukimbilia vitendo vya kimaada dhidi ya watawala au dhidi ya wale waliopinga da’wah yake, kikifuata mfano wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ambaye alijizuia Makkah pekee kwa da’wah na yeye (saw) hakufanya vitendo vyovyote vya kimaada mpaka alipohamia Madinah. Na wakati watu wa kiapo cha pili cha 'Aqaba walipopendekeza kwamba awape ruhusa ya kupigana na watu wa Mina kwa upanga, aliwajibu akisema: “Bado hatujaamrishwa kufanya hivyo”. Na Mwenyezi Mungu (swt) alimwomba (saw) kuwa na subira juu ya mateso kama Mitume wa Mwenyezi Mungu kabla yake walivyokuwa, wakati Mwenyezi Mungu (swt) alipowaambia:

“Na hakika walikanushwa Mitume kabla yako, na wakasubiri juu ya kukanushwa na kuudhiwa, mpaka nusura yetu ilipowafikia.” [TMQ 6:34]

Ukweli kwamba Chama hakitumii nguvu za kimaada kujilinda au kama silaha dhidi ya watawala hauhusiani na somo la jihad, kwa sababu jihad inapaswa kuendelea mpaka Siku ya Kiyama. Kwa hivyo wakati wowote maadui makafiri wanaposhambulia nchi ya Kiislamu inakuwa lazima kwa raia wake Waislamu kumfukuza adui. Wanachama wa Hizb ut-Tahrir katika nchi hiyo ni sehemu ya Waislamu na ni wajibu kwao kama ilivyo kwa Waislamu wengine, katika uwezo wao kama Waislamu, kupigana na adui na kumfukuza. Wakati wowote kukiwa na amiri Mwislamu anayetangaza jihad ili kukuza Neno la Mwenyezi Mungu (swt) na kuhamasisha watu kufanya hivyo, wanachama wa Hizb ut-Tahrir wataitikia katika uwezo wao kama Waislamu katika nchi ambayo wito mkuu wa silaha ulitangazwa.

Kutafuta Nusra (Msaada)

Wakati jamii ilipokosa kuitikia Chama kutokana na kupoteza imani kwa Ummah kwa viongozi na wakuu wake ambao uliweka matumaini yake kwao, mazingira magumu ambayo kanda hiyo iliwekwa ili kurahisisha utekelezaji wa njama, dhuluma na kukata tamaa ambayo watawala walifanya dhidi ya watu wao na madhara makubwa ambayo watawala walisababisha kwa Chama na wanachama wake, wakati jamii ilipokosa kuitikia kwa sababu hizi Chama kilianza kutafuta msaada wa watu wenye ushawishi kwa malengo mawili akilini:

  1. Kwa lengo la ulinzi, ili kiweze kufanikiwa kuendeleza da’wah yake kikiwa salama kutokana na mateso.

  2. Kuchukua utawala ili kusimamisha Khilafah na kutekeleza Uislamu.

Mbali na kufanya vitendo vya kutafuta msaada wa kimaada, Hizb inaendelea kufanya vitendo vyote ambavyo ilikuwa ikivifanya, kama halqa zilizokolea, uelimishaji wa pamoja, kuzingatia Ummah ili kuufanya ubebe Uislamu na kusimamisha maoni ya umma kwa ajili ya Uislamu ndani yake. Kiliendelea kupambana dhidi ya mataifa ya kikoloni ya kikafiri kwa kufichua mipango yao na kufichua njama zao, kama kilivyoendelea kupambana dhidi ya watawala kwa kuchukua maslahi ya Ummah na kutunza mambo yake.

Chama bado kinaendelea na kazi yake na kinatumai kwamba Mwenyezi Mungu (swt) atakiruzuku na kuuruzuku Ummah wa Kiislamu msaada, mafanikio na ushindi, na wakati huo waumini watafurahi.